Search This Blog

Wednesday 28 September 2016

FAIDA ZA KULA MATANGO (CUCUCMBERS)KUTIBU MARADHI NA KUTUMIKA KWA UREMBO


FAIDA ZA KULA MATANGO (CUCUCMBERS)KUTIBU MARADHI NA KUTUMIKA KWA UREMBO


Tango ni tunda moja wapo yenye maji mengi kama vile tikiti maji ,linabeba virutubisho vingi vitamin K,B,C,potasium,manganese .

image

Tango lina polyphenols ambayo inasaidia kukuepusha kupata maradhi sugu.Ni vizuri mkatumia matanga mara kwa mara kwa kutengeneza juice,kuchanganya kwenye kachumbali (salad)bila kumenya  maganda yake yanabeba virutubisho vizuri,au unaweza weka kwenye mkate na kuchanganya na maji ya kunywa kuyapa ladha na vitamins.




Umuhimu wa kula tango kwa afya yako


1.Kuipa kinga ubongo

Tango lina anti-inflammatory flavonol inayopelekea kuipa kinga ubongo na kukufanya kuwa na kumbukumbu nzuri (improve your memory).


2.Kupunguza hatari ya kupata cancer.

Tango linakupunguzia hatari ya kuapata cancer ya maziwa na shemu za uzazi (uterine,mayai ya uzazi (ovari).


3.Kutoa harufu mbaya mdomoni.

Kata kipande cha tango weka mdomoni kwa dakika 5 fanya mara 3 kwa siku inataidia kutoa bakteria wafanya kunuka mdomo .


4.Kupunguza stress

Tango linavitamins B,vitaminB1 vitaminB5 na vitamini B7 ambazo zinakupunguza stress.


5.Kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

Tango lina maji maji na fiber inayosaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni,kwa wale wenye  tatizo la kupata haja kubwa(constipation) kula tango bila kumenya ganda lake, linabeba fiber itakayo kusaidia kuapa choo kwa urahisi.



6.Wenye matatizo ya moyo

Tatizo la pressure linaweza kupunguzwa kwa kula matango mara kwa mara sababu tango lina potasium inayofanya kushuka pressure kwa urahisi na salama.


7.Kupunguza  hatari ya kupata kisukari,kupunguza cholesterol

8.Kutibu maumivu ya viungo

9.Kufanya kuwa na ngozi laini na kukuza nywele kwa haraka.


10.Kupunguza uzito


image

11.Kutumika kutoa alama nyeusi chini ya macho

Kata tango umbo la duara weka kipande kimoja kwa kila jicho, fanga macho ndio uweke kwa juu . Kwa matumizi ya uso(facial ) pia unasaga iwe laini (puree) na paka usoni acha kwa dakika 20 ,kish nawa kwa maji safi itakufanya kuwa soft na fresh.


12.Kutoa sumu mwilini

tengeneza juice ya tango,unaweza changanya na apple,spinachi na limao saga pamoja ni njia nzuri ya kutoa sumu mwilini kwa wale wanaotumia madawa kali 


Prepared by 
Dr Salim Amour
      Cardio_thoracic surgeon

No comments:

Post a Comment