Search This Blog

Wednesday 21 June 2017

ZIFAHAMU AINA YA DAWA 12 SALAMA KWA WAJAWAZITO




 

 makala zangu nyingi sana nimekua nikigusia swala la wajawazito na kukusisitiza kwamba watu hawa hawatakiwi watumie dawa yeyote bila kuandikiwa na daktari, niliwahi kuandika kuhusu dawa hatari kwa watu hawa
,...leo nakuja na dawa ambazo ni salama kwao, zipo nyingi sana ila ntataja zile muhimu tu ambazo zinatumika sana na zinapatikana kwenye mazingira yetu kama ifuatavyo;

penicillin; hili ni group la dawa za kuua bacteria au antibayotiki, hutumika kutibu magonjwa mbalimbali kwa mama mjamzito kama uti, kikohozi, magonjwa ya ngozi, na mengine mengi mfano ampicillin, cloxacilin, benzyl penicilin, pen v, benzathine peniciline na amoxycilline.

cephalosporins; hizi ni dawa zenye nguvu sana kuliko hizo nilizotaja hapo juu, hapa nchini hutumika kwa magonjwa ambayo mara nyingi yanakua yameshindikana kutibu magonjwa niliyotaja hapo juu mfano wa dawa hizo ni cefriaxon au powercef na cefuroxime.

macrolides; huu ni mchanganyiko wa dawa unaotibu na kuua bacteria mbalimbali wanaoshambulia mwili wa binadamu, hutumika kipindi cha ujauzito bila hofu mfano erythromycin, clarythromycin au clarinta na azithromycin au azuma.

paracetamol; hii ni dawa ya maumivu ambayo hutumika sana kipindi cha ujauzito, dawa zingine kama aspirin, diclofenac na diclopa hua hazitolewi kwa hofu ya kusababisha kuvuja sana kwa damu kwa mama huyu.

hydrocortisone cream; hii ni dawa inayotumika kutibu miwasho na aleji mbalimbali ni salama kwa mama mjamzito lakini haitakiwi kutumika kwa muda mrefu sana.

anusol; hizi ni dawa zinazotumika kutibu miwasho, maumivu au ugonjwa wowote sehemu za haja kubwa, haina madhara yeyote kipindi cha ujauzito. matatizo kama bawasiri au haemorroids huweza kutibika na dawa hii.

cotrimazole cream; hii ni dawa ya kutibu fangasi za aina mbalimbali kama za ngozi, uke na kadhalika, huweza kutumika kipindi cha ujauzito.

ducolax; hii ni dawa kwa ajili ya kutibu tatizo la kupata choo laini, kama mgonjwa anasumbukiwa na tatizo la kutoa choo ngumu sana dawa hii ni msaada mkubwa.

ranitidine; hii ni dawa ya kutibu madonda ya tumbo lakini pia hutumika kutibu gesi au kiungulia tumboni.

kwinini; hii ni dawa ya malaria ambayo ni salama kipindi chote cha ujauzito kwanzia mwanzo mpaka mwisho, dawa ya mseto ya malaria ni hatari sana miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito hivyo isitumike kipindi hicho.

cylindamycin; mara nyingi hufanya kazi zinazofanyika na fragile au metronidazole na ni mbadala mzuri kipindi hiki kwani fragile haifai kwa wazazi.

mebendazole; hii ni dawa nzuri sana kwa minyoo kipindi cha ujauzito, haina madhara yeyote, epuka matumizi ya albendazole kwani huweza kutoa mimba

2 comments:

  1. God bless Doctor abaka for helping me cure my herpes disease. Brethren, i have suffered herpes for a long period of time, i have tried so many remedy, but known seems to work. But i had contact with a herbal doctor who i saw so many people testifying on how they were all cured of their various disease and viruses by this doctor. So i explained my entire problem to him, and he promised to cure me. So i gave him all benefit of doubt, and behold he prepared the herbal mixture, and send it to me in my country. Today, i am proud to say i am herpes free, and my life has been restored to normal. So in case you are out there suffering from herpes and other diseases or virus, i want to tell you to quickly contact: abaka for your cure. His email is drabakaspelltemple@gmail.com or call +2349063230051.

    ReplyDelete

  2. The best herpes remedy, email [robinsonbucler@] gmail com.................

    ReplyDelete