📚 Ulimi wa mtu kwa kawaida hautakiwi kuwa na mipasuko ya aina yoyote . Sasa hawa watu wenye ulimi uliopasuka huwa hawana maumivu , isipokua tu labda kama kuna chakula kimekwama kwenye hiyo mipasuko ndio muhusika atahisi maumivu
📚 Mipasuko hii huweza kuwa iliyochimbika sana au kiasi tu.Wazee ndio hupatwa sana na hii mipasuko ya ulimi , japo yeyote yule anaweza kuwa na ulimi wa hivi.
Wanaume ndio huwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake
📤 NINI HUSABABISHA HALI HII ?
Hadi sasa , wataalamu hawajui ni nini hupelekea hali hii ya mipasuko kwenye ulimi , japo ina amini kwamba watu wenye undugu (genetics) huweza kuwa na tatizo hili na wengine wasiwe nalo . mfano katika familia , unaweza kuta mzazi ana tatizo hili na watoto pia
.
Mfano : Kuna tafiti ilifanyika na ikabaini kwamba watu wa South Africa ni 0.6% tu ya watu wote ndio wana tatizo hili la mipasuko kwenye ulimi , lakini Katika Taifa la Israel 30.6% ya watu wote ndio wana hii hali. Sasa unaweza ona kwamba swala la jamii fulani yenye mfanano wa kigenetiki huweza kuwa na hii hali ya mipasuko na jamii nyingine isiwe nayo
📤 TATIZO HILI LA MIPASUKO KATIKA ULIMI HUWA NA UHUSIANO NA MAMBO KAMA HAYA :
☂ Geographic tongue
☂ Kuvimba kwa lips na uso kutokana na matatizo ya neva
.
☂ Upungufu wa virutubisho muhimu kwa mwili n.k japo hii huwa na mchango mdogo
MATIBABU
Tatizo hili kiufupi , halihitaji tiba , isitoshe kisababishi hakijulikani , .
📤 USHAURI
Ubaya wa hii mipasuko ni kwamba endapo chakula kitabakia kwenye hiyo mipasuko , itapelekea bacteria kuzaliana , maumivu na hata kupelekea harufu mbaya ya kinywa na hata kuchangia meno kuharibika
Muhusika pia anakua katika mazingira marahisi ya kushambuliwa na fungus wa kinywa (candinda ablicans) , ikiwa imekutokea basi dawa zipo , onana na daktari
📚 Hakikisha unafanya usafi wa kinywa angalau mara mbili kila siku , na uwe na utaratibu wa kumuona daktari wa meno angalau mara mbili kwa mwaka
MWISHO NA ASANTENI 🙏
Am facing the same problem how can I get the medicines
ReplyDelete