Search This Blog

Saturday, 12 September 2020

BAWASIRI ( Hemorrhoids)

Bawasiri hutokea pale mishipa ya damu inapovimba au kuathiriwa kutokana na mgandamizo unaotokea katika sehemu ya chini ya puru.

Kuna aina mbili ambazo ni :

🌠 Bawasiri ya nje ; Hii hutokea ndani ya ngozi lakini katika sehemu ya nje ya tundu la haja kubwa (Anus)
.
🌠 Bawasiri ya ndani : Hii hutokea katika kuta za njia ya haja kubwa kwa ndani.

📤 Nini husababisha Bawasiri ?

Tatizo hili hutokea pale kunapokua na mgandamizo mkubwa katika mishipa ya damu (Veins) kuzunguka eneo la tundu la haja kubwa

Hili huweza sababishwa na mambo yafuatayo :

☂ Kukaa chooni kwa muda mrefu
.
☂ Tatizo la kuwa na haja kubwa ngumu kwa muda mrefu
.
☂Kuharisha sana kwa muda mrefu
.
☂ Kula vyakula visivyokua na nyuzinyuzi
.
☂ Kulegea kwa tishu maeneo ya tundu la haja kubwa (Hili husababishwa na swala zima la uzee au ujauzito )
.
☂ Kunyanyua vitu vizito mara kwa mara

📤Je , Dalili ni zipi ?

BAWASIRI YA NJE :

☂ Muwasho katika tundu la haja kubwa
.
☂ Uvimbe mmoja au zaidi pembezoni mwa tundu la haja kubwa
.
☂ Maumivu ya njia ya haja kubwa , hasa wakati wa kukaa

Swala la kujisafisha au kujikuna mara kwa mara kutaongeza tatizo liwe kubwa zaidi. Hali hii huweza kuisha ndani ya siku chache


BAWASIRI YA NDANI :

☂ Damu kutoka katika njia ya haja kubwa , hasa wakati wa kujisafisha au wakati wa kujisaidia
.
☂ Maumivu utayasikia wakati wa haja au unapobanwa na haja kubwa. Mara nyingi ni ngumu sana kuhisi maumivu hadi sehemu iliyoathirika itoke nje ya tundu la haja kubwa , yani kama kinyama hivi kutoka ndani ya puru


📤Je, Nikiwa nyumbani nawezaje kujitibu ?

☂ Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi

☂ Tumia dawa za kulainisha haja kubwa au virutubisho vyenye nyuzi nyuzi ( Fiber suppliments )

☂ Kunywa maji ya kutosha kila siku

☂ Usitumie nguvu kubwa kujisukuma wakati wa haja kubwa

☂ Usikae chooni muda mrefu (Hasa vile vyoo vya kukalia)

☂ Tumia dawa za kupunguza maumivu
.
☂ Chukua maji ya vuguvugu , yaweke kwenye beseni kisha utayakalia kwa dakika kadhaa , lakini unapoyakalia usikalie beseni yani njia ya haja kubwa ikusane na maji tu.



No comments:

Post a Comment