Search This Blog

Friday 16 October 2020

๐”๐•๐ˆ๐Œ๐๐„ ๐Š๐–๐„๐๐˜๐„ ๐Š๐ˆ๐™๐€๐™๐ˆ (๐’๐š๐›๐š๐›๐ฎ, ๐ƒ๐š๐ฅ๐š๐ฅ๐ข, ๐Œ๐š๐๐ก๐š๐ซ๐š ๐ง๐š ๐“๐ข๐›๐š )

 UVIMBE KWENYE KIZAZI (Uterine Fibroids)

Fibroids ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha unaoota na kukua kwenye mfuko wa uzazi ( uterus ) . Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji.

CHANZO CHA FIBROIDS

Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya msuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

 Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi. Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana

JE, DALILI ZA FIBROIDS NI ZIPI?
.
.
๐Ÿ“šAkina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zo zote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba.
.
.
Baadhi ya dalili za fibroids ni:
  • Kutokwa na damu kwa wingi au kutokwa na damu kwa muda mrefu
  • Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi
  • Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)
  • Kupata haja ndogo mara kwa mara
  • Maumivu ya mgongo
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku za hedhi
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu kwenye miguu
  • Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)
  • Mimba kutunga kwa shida
  • Kutopata mimba
  • Kutoka kwa mimba mara kwa mara

AINA YA FIBROIDS

Kuna aina nne za Fibroids

1. Intramural:

Fibroids aina hii hukua kwenye kuta za uterus. Hii ndiyo aina ya fibroids inayowapata wanawake wengi.

2. Subserosal fibroids:

Fibroids aina hii hukua nje ya kuta za uterus na huweza kuwa na shina. Subserosal fibroids huweza kukua na kuwa kubwa sana.

3. Submucosal fibroids:

Fibrioids aina hii huota na kukua kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za uterus.

4. Cervical fibroids: Fibroids aina hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

TIBA YA FIBROIDS

Kama mwanamke hapati usumbufu wa namna yo yote katika shughuli zake za kawaida, anaweza asipewe tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid kwa sababu mwanamke anapokaribia kukoma hedhi fibroids hunyauka zenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa. Lakini kama uvimbe unampelekea dalili mbaya za kumfanya ajisikie maumivu , au ashindwe kushika ujauzito n.k , basi tiba ni muhimu.
Endapo tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali iliyopo.

Tiba Ya Fibroids Kwa Kutumia Dawa

Tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina ya GnRHA (gonadotropin released hormone agonist) ambayo hutolewa kama sindano. Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka.
Tiba nyingine ni Tranexamic acid, vidonge vya kuzuia maumivu, vidonge vya kuzuia mimba (kuzuia mwanamke asipate hedhi) na LNG-IUS (Levonorgestrel intrauterine system) ambacho ni kifaaa cha plastiki kinachowekwa kwenye uterus.

Tiba Ya Fibroids Kwa Upasuaji

Kama dawa zimeshindwa kufanya kazi, mgonjwa hufanyiwa upasuaji kwa moja ya njia zifuatazo:

1. Hysterectomy– Kuondoa uterus.

Hii hufanywa pale fibroids zinapokuwa kubwa sana au pale ambapo mgonjwa anatokwa na damu nyingi sana. Upasuaji huu una madhara ya aina mbili: 1. Kupunguza hamu ya kufanya mapenzi 2. Kukoma hedhi mapema

2.Myomectomy– Fibroids kuondolewa kutoka wenye ukuta wa uterus.

Hii hufanyika pale ambapo mgonjwa anapenda kuendelea kuzaa. Tiba hii haoifanywi kwa fibroids kubwa au zile ambazo kwenye maeneo nyeti ya uterus.

3. Njia zingine, zinazoweza kutumika katika upasuji

USHAURI: IKIWA UNA DALILI ZOZOTE KAMA HIZO NILIZOZITAJA, SIO VIBAYA KUFANYA CHECKUP (VIPIMO) KWA AFYA YAKO ANGALAU HATA MARA MOJA TU KWA MWAKA

MWISHO NA ASNATENI

No comments:

Post a Comment