Search This Blog

Friday 16 October 2020

𝑺𝑨𝑹𝑨𝑻𝑨𝑵𝑰 𝒀𝑨 𝑼𝑲𝑬 (𝑪𝒉𝒂𝒏𝒛𝒐 , 𝑫𝒂𝒍𝒊𝒍𝒊, 𝑴𝒂𝒅𝒉𝒂𝒓𝒂 𝒏𝒂 𝑻𝒊𝒃𝒂)


 Saratani ya Uke hutokea mara chache sana kuliko saratani zingine. Huwa asilimia 1 tu kati ya saratani zote ambazo hutokea katika mfumo wa uzazi wa mwanamke

Kuna aina tatu za Saratani ya kizazi :

SQUAMOUS CELL VAGINAL CANCER

Aina hii ya saratani huanzia katika kuta za uke na kisha kuanza kukua taratibu . hii huwapata zaidi watu wengi ( 75%) ukilinganisha na aina zingine za saratani ya uke

 ADENOCARCINOMA

Aina hii ya Saratani huanzia katika tezi zilizomo katika uke . Huwapata zaidi wanawake wenye umri zaidi ya miaka 50.

MELANOMA na SARCOMA

Aina hizi pia huwapata wanawake katika seli zinazoipa ngozi rangi yake , na hiyo Sarcoma pia huanzia katika kuta za uke

Aina hizo zote za Saratani hutibika endapo zitagundilika mapema kuliko ambavyo zitakua zimesambaa sana

DALILI ZA SARATANI YA UKE

Dalili kuu ya Saratani ya Uke ni kutokwa na damu bila nyingi ukeni bila utaratibu maalumu. Mfano kutokwa damu sana baada ya kukoma kwa hedhi , kutokwa damu wakati au baada ya tendo la ndoa na kutokwa damu katikati ya mzunguko wako.

Dalili zingine ni kama vile :
  •  Kutokwa ute kama maji mara nyingi
  • Kukojoa mara kwa mara , na hata kupata maumivu wakati unakojoa
  •  Maumivu ya nyonga hasa wakati wa ngono
  •  Kupatwa na fistula , hasa pale Saratani inapokua katika hatua kubwa
  •  Wakati mwingine , Saratani ya uke , ni ngumu kujulikana na unaweza usipate dalili yoyote , ila hugundulika wakati wa vipimo

 NINI HUSABABISHA ?

Human papilloma Virus (HPV) . Kirusi huyu husambazwa kwa njia ya ngono na ndio msababishi mkuu wa Saratani ya uke

Kisababishi kingine ni Diethylstilbestrol (DES), Hii ni dawa ambayo hupewa mwanamke kuzuia mimba isiharibike . Japo matumizi yake yalishakomeshwa tangu miaka ya 1970's , kwahiyo kwa sasa dawa hiyo haitumiki hivyo sio kisababishi kwa kipindi hiki

MAMBO YANAYOWEZA KUCHANGIA UPATE KIRAHISI SARATANI YA UKE
  • Uvitaji sigara, hii huongeza uwezekano mara mbili zaidi
  • Kuwa na umri zaidi ya miaka 60
  • Kuwa na HIV
  • Kama ulishapata HPV hapo kabla kupitia ngono ( HPV pia husababisha masundosundo - Warts , kwahiyo kama ulishakua na masundosundo basi inakua rahisi zaidi kupata saratani ya Uke)

 Saratani ya uke imegawanyika katika Stage 4 (Hatua 4)

Hatua ya 1 : Hapa saratani inakua imeathiri ukuta tu wa uke

Hatua ya 2 : Saratani inakua imeathiri tishu baada ya uke , ila inakua haijafika kwenye maeneo ya ndani zaidi

Hatua ya 3 : Hapa saratani inakua imevuka mipaka na kuanza kuathiri maeneo ya nyonga na hata lymph nodes

Hatua ya 4: Hapa Saratani inakua imeenda mbali zaidi na kuathirizi maeneo mengine kama vile puru, kibofu cha mkojo na maeneo jirani . Hatua ya 4 - B , inakua imeenda mbali zaidi na kuathiri figo hata ini

MATIBABU YAPOJE ?

Upasuaji utahusika , hasa unapokua na saratani hatua ya 1 (Stage 1) kuondoa tishu kuzunguka eneo la uke lililoathirika. Itafuatiwa na Radiotherapy

Radiotherapy na Chemotherapy vinaweza husika pia . Radiation kwa kawaida hufanywa kulingana na eneo husika la mwili linalohitaji tiba

Hatua ya 4 B : Hii haiwezi tibika , ila njia hizo mbili za mionzi na dawa zitatumika tu kupunguza dalili au mathara unayoyapata kutokana na saratani hiyo


UFANYE NINI KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA TATIZO HILI ?

 Punguza uwezekano wa wewe kupata HPV , mfano tumia condom kujikinga
Fanya vipimo mara kwa mara ili kama tatizo lipo ligundulike mapema

 Acha kuvuta sigara , pia kuna ushahidi usio mkubwa sana unaosema unywaji wa pombe sana huweza changia

No comments:

Post a Comment