Search This Blog

Thursday 10 September 2020

𝑽𝑰𝑫𝑶𝑵𝑫𝑨 𝑴𝑫𝑶𝑴𝑶𝑵𝑰 𝑵𝑨 𝑻𝑰𝑩𝑨 𝒀𝑨𝑲𝑬 (𝑴𝒐𝒖𝒕𝒉 𝒖𝒍𝒄𝒆𝒓𝒔)

Vidonda vya mdomoni ( Mouth ulcers) huweza kupelekea muhusika kushindwa kufurahia chakula anachokula au hata maongezi nk

Vidonda vya mdomoni huweza kuwa vikubwa au vidogo kulingana na sababu zilizopelekea kidonda hicho , kwa kawaida vidonda hivi hupona kati ya siku 7 hadi 14 . Lakini endapo ni vikubwa huweza kuchukua muda mrefu kupona

📤 Je , SABABU ZINAZOPELEKEA VIDONDA VYA MDOMONI NI ZIPI?


🏺 Majeraha wakati wa kusafisha kinywa na majeraha mengine kama yanayosababishwa na ajali au wakati wa kupata huduma za kinywa kwa madaktari wa meno
.
🏺 Vyakula na asidi iliyomo , mfano Matunda kama limao nk yenye asidi nyingi huweza pia kusababisha vidonda
.
🏺 Ukosefu wa vitamin B-12, zinc , folate au Iron
.
🏺 Mabadiliko ya homoni kipindi cha hedhi
.
🏺 Mzio dhidi ya bacteria wa kinywa
.
🏺 Matumizi ya braces
.
🏺 Msongo wa mawazo na ukosefu wa usingizi
.
🏺 Maambukizi ya bacteria, fungi na virusi


📤 PIA VIDONDA VYA MDOMONI HUWEZA KUTUELEZA MATATIZO MAKUBWA YANAYOHITAJI MATIBABU YA HARAKA KAMA VILE ;


☔ Celiac disease ( Hutokea baada ya mzio wa kinga ya mwili dhidi ya Gluten , kisha villi huathiriwa au kuharibiwa , kiufupi ni tatizo katika mfumo wa chakula , kisha sehemu zingine za mwili pia huathiriwa)
.
☔ Inflammatory bowel disease
.
☔ Behcets disease
.
☔ Kisukari
.
☔ Ukimwi
.
☔ Kinga ya mwili inaposhambulia seli katika tishu mbalimbali badala ya kushambulia bacteria , au virusi


📤 HIZI NI NJIA BAADHI YA KUTIBU TATIZO HILI LA VIDONDA VYA MDOMONI ;

☔ Sukutua kwa maji ya chumvi au baking soda
.
☔ Kuweka (Milk of magnesia ) katika vidonda - Utazipata pharmacy
.
☔ Kutumia bonzocaine - Mfamasia atakuelekeza
.
☔ Tumia virutubisho vyenye vit B-12 , B-6 , iron, zinc, folic acid


📤 Zingatia ya fuatayo kuepuka tatizo ;

🏺 Kama tatizo lilitokana na kutumia sana vyakula au matunda yenye asidi nyingi basi punguza matumizi yake
.
🏺 Zingatia usafi wa kinywa kila siku
.
🏺 Kula mlo kamili
.
🏺 Pata usingizi wa kutosha
.
🏺 punguza stress

📤 USHAURI ; Ikiwa vidonda ni vikubwa na unapata maumivu sana , zipo dawa za kupunguza maumivu . Ikiwa una bacterial au viral infection Onana na daktari uanze matibabu , dawa zipo


USIKAE MDA MREFU NA HIVO VIDONDA , MAANA BAADAE ITAKUA NGUMU SANA KUTIBIKA , NA VINAWEZA SABABISHA CANCER , KUNA WATU WANAKAA NA HIVYO VIDONDA KWA MIAKA , NI HATARI

2 comments:

  1. Mimi Nina kinyama mdomoni haliumi Ila kipo MDA mrefu n Kama kiuvimbe tu sijielewi nifanyaj?

    ReplyDelete
  2. The best herpes remedy, email [robinsonbucler@] gmail com

    ReplyDelete