Search This Blog

Friday, 5 August 2016

FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUWI BADO

Huwa inanishangaza sana ninapoutafakari ukuu wa Mungu kwa namna ambayo ametupa mimea mbalimbali mhimu kwa ajili ya afya zetu – Mwanzo 1:29. Maelezo yafuatayo kuhusu tangawizi  yatakupa wewe ujuzi wa mmea mwingine wa asili usio na madhara ya kikemikali na kusaidia mwili wako kuwa na afya nzuri na ya kupendeza.

Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa mhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kudili na aina mbalimbali za kansa mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.

Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza radha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadharika. Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.

Tangawizi ni zao la kibiashara na ni rahisi kutoka kimaisha kama utaamua kulima tangawizi ingawa ni zao la miezi mingi lakini ukivumilia utakula bata tu, gunia moja linauzwa kati ya laki 3 hadi 6 wakati wa msimu mzuri.

Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.

Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.

Leo nimekuletea hii juisi ya tangawizi, nimetumia tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Kazi 48 za tangawizi mwilini

1. Huondoa sumu mwilini haraka sana

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi

4. Huondoa uvimbe mwilini

5. Huondoa msongamano mapafuni

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake

7. Huondoa maumivu ya koo

8. Huua virusi wa homa

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi

19. Huongeza msukumo wa damu

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha kolesto

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa

25. Hutibu shinikizo la juu la damu

26. Husafisha utumbo mpana

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

34. Husaidia kuzuia kuharisha

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto

37. Hutibu homa ya kichwa

38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

41. Huimarisha afya ya figo

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi

43. Ina madini ya potassium ya kutosha

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

Like ukurasa huu wangu kwa makala nyingine kali kama hii

No comments:

Post a Comment