Search This Blog

Thursday 4 August 2016

DALILI 10 ZA KUSHIKA MIMBA


Dalili kumi za kukujulisha kuwa umeshika
mimba
Hutokea mara nyingi kina mama na wasichana
kuwa na kipindi cha msongo wa mawazo pale
wanapokosa siku zao na hasa kama
hawakutumia njia ya uzazi wa mpango au
kinga nyingine ya kushika mimba.
Kukosa siku zako sio dalili pekee ya kushika
mimba, bali kuna dalili zingine utalazoziona.
Kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza
kukufanya ukose siku zako, hivyo soma dalili
za mimba ili ikusaidie kupata uhakika.

Moja, ni mabadiliko katika siku zako. Hii
kitaalamu tunaita spotting. Unaweza kushika
mimba ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii
hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza
kwenye kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa
kwenye ukuta huu tayari kulisha kiumbe
huachia damu kidogo amabazo mwanamke
anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida.
Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani
kiwango na siku za damu hubadilika.

Pili, ni kuongezeka ukubwa na kupata maumivu
kwenye maziwa. Hii inasababishwa na ongezeko
la homoni za istrogen pale unapokuwa umeshika
mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi
mitatu ya kwanza.

Tatu, ni kichefuchefu na kutapika. Hali hii
huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi
unapoToka kulala. Hii ni kwa sababu ya homoni
ya ‘projestroni’ ambayo husababisha
kupungua nguvu kwa misuli ya mrija wa
chakula au koromeo.

Nne, ni uchovu usiokuwa na usingizi usiokuwa
na sababu. Hii hutokea kwa sababu ya ongezeko
la homoni ya ‘projestroni’ na mama utajikuta
unasinzia mara kwa mara. Hali hii huisha
unapoanza mwezi wa nne wa mimba ila hata
kipindi cha mwisho wa mimba hujisikia uchovu.

Tano, kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hasa
kama unapata mimba kwa mara ya kwanza,
utachukia harufu za vyukula na vinywaji
mabalimbali. Wakati mwingine hata harufu za
watu walio karibu nawe zinaweza kukukera.

Sita, ni kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya
nguo zako zinakubana zaidi hasa sehemu ya
tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi
mwilini zinazokufanya kijisikia tumbo kujaa.

Saba, Kukojoa mara kwa mara. Hii kwanza
hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini
ambayo huongezwa na homoni za ujauzito
makusudi kutoa rishe ya kutosha kwako na kwa
kiumbe tumboni. Ukiwa na damu nyingi pia
utakojoa sana za kikemia mwilini. Pili
utajisikia kwenda haja ndogo mara nyingi pale
kiumbe kitakapoongezeka na kubana kibofu cha
mkojo.

Nane, kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa kina
mama ambao hupima joto lao kama njia ya
uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto
limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na
nusu mfurulizo.

Tisa, kutoona siku sako kabisa. Kwa wale ambao
siku zao hazibadiliki na huenda vizuri
yawezekana kugundua pale wanapokose siku
nap engine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa
wale ambao siku zao hubadilika sana wataona
kawaida ila kama ameshika mimba taona
mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu na
kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

Kumi, kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha
karatasi ngumu. Famasi nyingi huuza vipimo
ambavyo ikikichovya kwenye mkojo wako huweza
kugundua homoni za mimba kwenye mkojo.
Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani
hata kazini. Kipimo hiki ukisha kichovya kwenye
mkoja kama katatsi inavyoelekea utaona
mistali baada ya dakika moja inajitokeza
upande wa chini.
Ikitokea mistari miwili basi unaweza kuwa na
mimba na ukitokea mmoja utakuwa huna
mimba. Kilingana na kiwango cha homoni
mwilini, kuna kina mama hakionyeshi majibu
mpaka upitishe wiki moja bila kuona siku zako.

Pamoja na dalili hapo juu, unatakiwa kupata
ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.  

Prepared by Dr Salim Amour
       Cardio_thoracic Surgeon

No comments:

Post a Comment