Search This Blog

Thursday 4 August 2016

HEDHI NA MZUNGUKO WAKE



NINI MAANA YA MZUNGUKO WA HEDHI???
mzunguko wa hedhi ni mzunguko wa kila mwezi ambao husababisha kutokwa kwa damu ukeni kutokana na mimba kutotungwa,


Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni 

(1)MZUNGUKO WA DAMU UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hutokwa na ute ute wa Uzazi ambao unavutika na mwanamke huyu huweza kupata mimba,

(2)MZUNGUKO WA DAMU USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hatokwi na ute ute wa Uzazi hivyo huwa hawezi kupata mimba
~pamoja na mizunguko hii kutofautiana mwanamke hupata hedhi kama kawaida, hata hivyo mwanamke ambaye mzunguko wa hedhi yake apati ute wa Uzazi hawezi kupata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni
~ute ute wa Uzazi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni (1)UTE MWEPESI
(2)UTE UNAOVUTIKA
(3)UTE MZITO

~Mara nyingi wanawake wasiopevusha mayai hawawezi kupata ujauzito hivyo huwa hawapati ute wa Uzazi, na wengine hupata ute mzito daima kama uchafu unaotoka ukeni Lakini wenyewe hauna harufu wala muwasho
JINSI YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
~Kila mwezi ovari za mwanamke huzalisha yai moja ambalo Lina uwezo wa kukaa kwa muda wa masaa 36 ndani ya mirija ya Uzazi hivyo inapotokea yai hili halijarutubishwa ukuta wa mji wa Uzazi hubomoka na kutoka nje ya uke pamoja na damu hvyo kwa neno Moja tunasema siku za hedhi
~mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa siku ya kwanza mwanamke anapoanza kupata siku zake
~mzunguko wa hedhi uwe unapevusha mayai au haupevushi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni 

(1)MZUNGUKO MFUPI ~mzunguko huu huwa Kati ya siku 22_27

(2)MZUNGUKO MREFU ~mzunguko huu ni wa siku 31_35 

(3)MZUNGUKO WA KAWAIDA ~mzunguko huu huwa na siku 28_30
MFANO :JINSI YA KUSOMA MZUNGUKO WA KAWAIDA 
Siku ya kwanza mpaka ya tano huwa ni kipindi cha mwanamke kuingia katika hedhi huo ni mwanzo wa mzunguko wa hivyo kipindi hiki ukuta wa mji wa Uzazi hubomoka na kutoka na kutoka damu ukeni, katika kipindi cha Sita hadi ya kumi huwa ni kipindi ambacho ukuta wa Uzazi huanza kujengwa Tena na yai huundwa kwa ajili ya kupokea kiini tete katika kipindi hiki homoni ya estrogen huwa nyingi, pia katika kipindi hiki yai huzalishwa (ovulation) siku ya kumi na moja mpaka kumi na nane ya mzunguko pia yai Hilo huweza kukaa kwa muda wa masaa 36 yani hutoka katika ovari na kusafiri katika mirija ya falopia mpaka siku ya kumi na tisa hadi 28  hapo homoni za progesterone huzalishwa kwa wingi kwa ajili ya kutunza mji wa mimba pia homoni za progesterone hupungua mwishoni mwa mzunguko yani kupungua huku husababisha mwanamke kuingia 
Tena katika mzunguko wa damu 
~mwanamke hupata hedhi yenye rangi nyekundu na huwa Ina mabonge kiasi kidogo na hutoka kiasi cha ML 35_50 kwa saa 
Hata hivyo pamoja na watu kupenda kuona siku zao ili kuondoa wasiwasi wa mawazo yao kama wamebeba mimba pasipo kutarajia pia kuna watu wanachukia kuona siku zao kutokana na maumivu au adha wazipatazo miongoni mwa shida hizo ni KUPATA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI, KUTOPATA HEDHI KATIKA MPANGILIO ULIO SAHIHI, KUHISI KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA, KUPATA FLOW KUBWA SANA   mada inayokuja tutazungumzia jinsi yakuweza kuzuia 

Prepared by Dr Salim Amour 
Cardio_thoracic Surgeon

No comments:

Post a Comment