MAGONJWA ya Moyo (Cardiovascular Diseases), ni miongoni mwa magonjwa yaliyoko kwenye kundi la ugonjwa usioambukiza. Haya ni magonjwa yale yote yanayoathiri moyo na mishipa yake. Kwa hiyo, magonjwa ya moyo yanajumuisha ugonjwa wa Kupanda kwa Shinikizo la Damu (High Blood Pressure/Hypertension). Hili ni tatizo sugu la kiafya linalohusisha kuongezeka kwa mgandamizo wa msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu.
Welcome to Salim healthcare that delivers relevant information in clear, free language that puts health into context in peoples' lives. Through medical content, insights from experts and real people, and breaking news, we answer: how it happened, what it feels like, what you can do about it, and why it matters.
Search This Blog
Thursday, 29 September 2016
FAIDA 27 ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA ASALI NA MDALASINI

SIKU YA MOYO DUNIANI SEPTEMBER 28
World Heart Day: 7 healthy diet and exercise tips for a healthy heart
Nutritionists explain how a healthy diet and lifestyle can benefit your heart.
Many of us would think twice before saying no to a delicious, hearty meal any time of the day. Only thing is, we tend to overlook an important aspect the moment we lay our eyes on a sumptuous spread — the harmful effects food can have on our health and more specifically, our heart.

Wednesday, 28 September 2016
FAIDA ZA KULA MATANGO (CUCUCMBERS)KUTIBU MARADHI NA KUTUMIKA KWA UREMBO

Posted by Dr Salim Amour
FAIDA 10 ZA TENDE
TENDE NI TUNDA
Tende ziko za aina mbili kavu na mbichi. Tende ina sukari kiwango cha asilimia 60 – 70 na pale inapopigwa na jua hupunguza uzito wa asilimia 35.

Faida za kula tende
Tende ni dawa nzuri inayosaidia usagaji wa chakula tumboni, huongeza nguvu ukila tende na maziwa ni vizuri sana kwani huongezeka mwendo wa damu, kusafisha damu na pia ni nzuri ukimpa mtoto anayekua kuanzia umri wa miaka 7 na kuendelea.
Usumbufu wa tumbo, hii hutokana na vijidudu tofauti kwa mfano minyoo huchangia tumbo kuuma sana pia vidudu vengine (bacteria). Tende huuwa vijidudu vyote vinavyosababisha kuumwa na tumbo. Asubuhi kabla hujala kitu chochote kila siku kula kokwa moja la tende hii husaidia kuua wadudu watumbo ambao wanasababisha harufu mbaya kinywani.
Hutibu maradhi ya moyo. Loweka tende usiku mzima katika maji na unywe maji yake asubuhi huepusha maradhi ya mshtuko wa moyo mara kwa mara na fanya hivo mara mbili kwa wiki.

Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni madini na vitamini lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya.
Katika makala ya leo, nimekuorodhoshea faida zake 10:

1 .Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamini za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat) na haina lehemu (kolestrol).
2.Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla.
3.Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.
4.Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’.
Ili kupata faida zaidi za tende, changanya na maziwa fresh kisha kula. Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wanaofunga, ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima.

Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL Cholesterol).
5.Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini.

6.Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.
Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.

7.Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.
8.Tende inatibu saratani ya tumbo. Habari njema kuhusu tende kama tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
9.Kwa ujumla faida za tende ni nyingi na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizi 10 na nyingine.
Prepared by
Dr Salim Amour
Cardio_thoracic surgeon
STRESS
Do I have depression?
Clinical depression is an illness that affects millions of people – yet is often difficult to diagnose and treat. Many people who experience depression are reluctant to admit to it, seeing the illness as a sign of weakness or something that will pass. The distinction between feeling down and being clinically depressed is often difficult
Signs of Depression
Clinical depression is an illness that affects millions of people – yet is often difficult to diagnose and treat. Many people who experience depression are reluctant to admit to it, seeing the illness as a symbol of weakness or something that will pass. Acting upon the signs of depression is a vitally important step. The distinction
How to deal with stress at work
Stress at work can come from a number of sources. As you get older, the longer hours can start to weigh heavy on you and cause physical, as well as mental, tension. Even if you’ve decided to cut back on your hours in an attempt to shift your work-life balance, it could be that you’re […]
Simple relaxation techniques
Stress doesn’t have to take over. With these simple tips, you can reduce your stress levels and enjoy a happier life. What stress? While a lot of us don’t like to admit it, there are a number of things in life that get us stressed. These include problems at work and financial worries; bedroom issues
Does stress cause hair loss?
In order to answer this, we need to look at the different types of hair loss. First up is male pattern baldness. This tends to be a genetic condition and is related to family traits and old age. With this form of hair loss – called androgenic or androgenetic alopecia – hair usually recedes along
How to keep your stress levels down
Stress and anxiety can cause a number of health issues, which leads to a vicious circle – you get stressed, which causes sickness, which makes you more stressed and so on. It can also sneak up on you little by little until suddenly you feel like you can’t cope. However, by tackling the initial cause
"Not Tonight, Dear": Men Avoid Sex Too
The ‘not tonight, dear, I’ve got a headache’ stereotype is one that has endured mainly because it has some truth to it. However, it’s not just women who sometimes want to avoid sex. Men do it too – it’s just talked about less because of the ‘macho myth’ that men constantly think about sex.
Overcoming Sexual Performance Anxiety
Whether you’re a modern-day Casanova or a one-woman man, at some point in your sex-life you may start to suffer from sexual performance anxiety. It could be due to stress, growing older, an illness, or your body image, but once you start to worry about your sexual performance it can become a vicious circle
Saturday, 17 September 2016
FAHAMU KUHUSU CANCER (SARATANI)
KANSA au kwa jina jingine, Saratani, ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu za mwilini. Kansa isiyotibiwa, inaweza kuwa ugonjwa unaoshambulia tishu nyingine mwilini na kusababisha kifo.
Kwa kawaida, kansa huusababishia mwili madhara pale inapoharibu seli na kuzifanya zigawanyike bila kudhibitika na kuwa uvimbe wa tishu unaojulikana kama tumor, isipokuwa katika kansa ya damu ambapo kansa huzuia utendaji wa kawaida wa damu kwa kuzifanya seli ziwe na mgawanyiko usio wa kawaida katika damu.
Ni nini chanzo cha ugonjwa wa kansa?
Mwili wa binadamu umeundwa kwa trilioni za seli ambazo hukua, kugawanyika na kufa kwa mpangilio maalumu. Mwenendo ulioratibiwa vyema unasimamiwa na vinasaba (DNA) vilivyo ndani ya seli. Vinasaba hivyo, vinapatikana katika kila seli, na huongoza matendo yote yanayofanywa na seli. Katika seli ya kawaida, wakati vinasaba vinapoharibika, seli hukarabati au seli hufa.
Lakini katika seli za kansa, kinasaba kilichoharibika huwa hakiwezi kukarabatiwa na seli haifi kama inavyotakiwa, badala yake huendelea kutengeneza seli nyingine ambazo hazitakiwi na mwili na hivyo seli hizo mpya zote huwa na kinasaba kisichokuwa cha kawaida tofauti na seli salama.
Watu huweza kurithi kinasaba kisichokuwa cha kawaida, ingawa mara nyingi uharibifu wa kinasaba husababishwa na makosa yanayotokea wakati seli ya kawaida inapotengenezwa au kutokana na sababu za kimazingira. Ingawa inajulikana wazi kwamba kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kuharibu kinasaba na kusababisha kansa, kama vile kemikali, uvutaji sigara, kuchomwa na jua na kadhalika, lakini bado hakuna uhakika wa moja kwa moja kuhusiana na kinachosababisha kansa.
Wakati mtu anapokuwa mtoto mdogo au bado akiwa ndani ya tumbo la mama, seli hujigawanya kwa haraka ili kumfanya akuwe.
Baada ya mtu kukua, seli nyingi hugawanyika kwa ajili ya kuchukua nafasi ya zile zilizozeeka na kufa au kwa ajili ya kukarabati majeraha.
Kansa huanza wakati seli katika sehemu mojawapo ya mwili zinapoanza kukua bila kudhibitiwa. Ukuaji wa seli za kansa hutofautiana na ukuaji wa kawaida wa seli za mwili, na badala ya kufa pale zinapozeeka, zenyewe huendelea kukua na kuzaa seli nyingine mpya zisizokuwa za kawaida.
Seli za kansa pia hushambulia kwa kuingia ndani ya tishu nyigine jambo ambalo halishuhudiwi katika seli za kawaida. Kwa kawaida seli za kansa husambaa katika sehemu nyingine za mwili ambako huko nako, huanza kukua na kuunda uvimbe (tumor) mpya na baada ya muda kupita uvimbe huo huchukua nafasi ya tishu mpya.
Kwa hiyo, kukua kusikodhibitiwa na kusiko kwa kawaida kwa seli, na tabia ya seli hizo kuzishambulia tishu nyingine, ndiko hasa husababisha seli za kansa.
Sifa za ugonjwa wa kansa
Si kila uvimbe ni kansa, bali kuna uvimbe ambao si kansa, ambao kitaalam huitwa 'Benign Tumors', kama vile Tezi dume (Benign Prostate Hyperplasia). Uvimbe huweza kugawanyika na kukua, na pia hutengeneza mirija mipya ya damu ili kujipatia lishe wenyewe. Kitendo hiki kitaalam huitwa 'Angiogenesis.'
Hata hivyo, uvimbe huu usiokuwa kansa, unaweza kuleta matatizo kama vile kukua sana na kuvibana viungo na tishu nyingine mwilini. Aidha, uvimbe kama huu, huweza kukua na kuingilia mifumo ya umeng'enyaji, fahamu na damu/limfu na huweza kutoa homoni zinazobadili utendaji wa kawaida wa mwili.
Ingawa uvimbe usiokuwa kansa unaweza kuwa hatari kwa afya, lakini hauwezi kuzishambulia seli nyingine au kusambaa katika viungo vingine mwilini. Uvimbe wa aina hii, mara nyingi hutibika na huwa hauhatarishi maisha.
Hata hivyo, aina zote za kansa zina sifa tatu zinazofanana. Sifa hizo ni ukuaji wa seli usiodhibitika, uwezo wa kuvamia na kushambulia tishu nyingine na uwezo wa kusambaa katika viungo vingine mwilini kupitia mishipa ya damu au mikondo ya limfu. Kitendo hicho cha vidudu vua ugonjwa wa kansa kusambaa mwilini kupitia mkondo wa damu na limfu, kitaalam huitwa 'Metastasis'.
Aina za kansa
Hadi sasa kuna aina zaidi ya 200 za kansa kulingana na kiungo gani cha mwili kimeathirika au eneo la mwili linaloshambuliwa.
Baadhi ya kansa huwashambulia zaidi wanawake, kwa mfano kansa ya matiti na kuna baadhi ambazo huwashambilia zaidi wanaume.
Baadhi ya kansa huwashambulia watu wa kundi fulani katika jamii kutokana na aina yao ya maisha au kazi wanazofanya kila siku, na hali kadhalika kuna baadhi ya kansa au saratani zinazoshambilia watoto zaidi kuliko watu wazima, kwa mfano kansa ya damu aina ya 'Lymphoblastic'.
Zifuatazo ni baadhi ya aina za kansa kulingana na tabia hizo hapo juu:-
- CARCINOMAS. Hii ni saratani ambayo hushambulia viungo mbalimbali vya mwili vilivyo ndani na nje, kwa mfano mapafu, matiti, utumbo na kadhalika.
- SARCOMAS. Hii ni saratani inayopatikana kwenye mifupa, misuli na tishu mbalimbali mwilini.
- LYMPHOMAS. Hii ni saratani zinazoanza kwenye mikondo na vifundo vya limfu na kwenye tishu za kinga ya mwili.
- LEUKEMIAS. Hii ni saratani zinazoanza ndani ya ute wa mifupa (bone marrow) na kukusanyika kwenye mishipa ya damu.
- ADENOMAS. Hii ni saratani zinazochomoza kwenye tishu na tezi zinazotoa homoni mbalimbali hasa tezi zilizopo kichwani.
Ni nini huchangia kuwepo kwa ugonjwa wa kansa?
Asilimia 60 ya magonjwa yote ya kansa yanahusishwa zaidi na mtindo wa maisha ambao vipengele vyake ni ulaji, mazoezi ya mwili na matumizi ya pombe na tumbaku. Vitu vingine vinavyochangia, ni pamoja na virusi na bakteria, madini mazito, mionzi na sumu kadhaa.
Vyakula huchangia kwa kiasi kikubwa saratani za kinywa na koo, matiti, tezi ya kiume, utumbo mpana, mapafu, tumbo, ini, kongosho na kizazi. Ulaji unaoweza kuchangia ugonjwa huu, ni pamoja na ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi, nyama zilizosindikwa, vyakula vilivyokuzwa kwa kemikali nyingi kama mbolea, vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huweza kusababisha uzito mwingi na vyakula vilivyoota ukungu, kwa mfano karanga.
Kitaalam, nyama nyekundu ni muhimu kwa binadamu, lakini inakuwa tatizo pale inapoliwa zaidi ya nusu kilo kwa wiki. Ulaji wa nyama nyekundu mfano ng'ombe, unaongeza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo mkubwa.
Tafiti zimeonesha kuwa kula nyama nyekundu hadi nusu kilo kwa wiki haiongezi uwezekano wa kupata saratani, lakini kila gramu 50 zinazoongezeka, huongeza uwezekano wa kupata saratani kwa asilimia 15.
Nyama zilizosindikwa pamoja na zile zilizohifadhiwa kwa kuongezwa chumvi, mafuta, kemikali au kukaushwa kwa moshi kama nyama za kopo, soseji na bekoni zinaongeza sana uwezekano wa kupata saratani. Hakuna kiasi chochote cha nyama iliyosindikwa kinachoweza kutumika bila kuongeza uwezekano wa kupata saratani.
Viazi vya kukaanga mfano viazi mviringo (ulaya), huongeza hatari ya kupata saratani hasa vikikaangwa kwenye mafuta yenye haidrojeni na lehemu. Viazi ni moja ya vyakula vyenye wanga sana na wakati wa kukaangwa hutoa 'Acrylamide' ambayo ni kisababishi cha kansa hasa kwenye mfumo wa fahamu.
Vinywaji baridi/Laini kama vile soda na juisi za viwandani navyo vinaweza kusababisha kansa. Utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Jarida la 'Cancer, Epidemiology, Biomakers & Prevention' unaonyesha kuwa mtu aliyetumia soda mbili au zaidi ndani ya wiki moja, ana uwezekano wa kupata saratani ya kongosho kwa asilimia 87 kuliko mtu ambaye hatumii kabisa vinywaji hivyo laini.
Hakikisha katika kila mlo unaotumia kunakuwa na nafaka zisizokobolewa kama vile unga wa ngano usiokobolewa sana, unga wa dona, mchele wa brauni, ulezi na kadhalika na aina mbalimbali za mikunde kama vile maharage, kunde, choroko na mbaazi.
Mazoezi ya mwili yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili ya wastani kama vile kutembea haraka haraka angalau dakika 30 kila siku, na mwili ukishazoea, unashauriwa kuongeza hadi kufikia dakika 60 kila siku.
Kama unafanya mazoezi ya nguvu sana, basi iwe angalau dakika 30 kila siku. Punguza sana mtindo wa maisha ambao unakufanya uketi bila mazoezi kama vile kuangalia televisheni kwa muda mrefu.
Tumia nafasi zote zilizopo za kuzoeza mwili kama vile kupanda ngazi badala ya kutumia lifti, kusaidia kazi za nyumbani, kutembea kwenda sokoni au dukani kama si mwendo mrefu na kadhalika.
Ni nini dalili za ugonjwa wa kansa?
Kwa kawaida saratani huanza taratibu, na huchukua muda mrefu kuonyesha dalili zake zote. Aidha, dalili za awali haziambatani na maumivu yoyote, hivyo kusababisha wagonjwa wengi kuchelewa kutafuta matibabu.
Magonjwa mengi ya saratani hutibika yakigundulika mapema. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), linaema asilimia 30 ya saratani zinaweza kuzuilika. Hivyo ni muhimu kwa kila mtu kumuona mapema mhudumu wa afya kila anapoona dalili zisizo za kawaida katika mwili wake, kama vile dalili za kutokwa na damu ukeni kwa mwanamke baada ya kufanya tendo la ndoa, baada ya kukoma mzunguko wa hedhi, au nje ya mzunguko wa hedhi.
Kukojoa mara nyingi zaidi ya kawaida au mkojo kutoka kwa shida; uvimbe wa zaidi ya wiki tatu shingoni, kwapani, tumboni, ngozi au matiti; kubadilika kwa kawaida ya kupata choo (kufunga choo); matiti kubadilika umbile, uvimbe, ngozi au kutoa maji maji.
Kukohoa au sauti ya kukwaruza kwa zaidi ya wiki tatu; shida au maumivu wakati wa kumeza chakula au vinywaji; kutokwa na damu kwenye choo, mkojo, makohozi au pua; kutokwa na ute, maji maji au usaha ukeni; uchovu bila kufanya kazi; kupungua uzito ghafla bila sababu na kukosa hamu ya kula chakula.
Jinsi ya kudhibiti kabisa kansa
Ikiwa kansa au saratani ishatokea na kuanza kusambaa mwilini, mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili kudhibiti usambaaji huo ni pamoja na kutibiwa kwa kufanya upasuaji, tibakemo (matibabu kwa dawa); kupata matibabu kwa njia ya eksirei (matumizi ya mnururisho wa kuweka ioni ili kuua seli za kansa na kunywea uvimbe); kupata matibabu ya tiba maradhi; kupata matibabu ya monokloni ya kingamwili au njia nyingine.

Subscribe to:
Posts (Atom)