Search This Blog

Sunday 23 October 2016

MATATIZO YA FIGO

Matatizo ya Figo na dalili zake.


VISABABISHI VYA UGONJWA WA FIGO
1.Matumizi mabaya ya dawa hasa za maumivu kama diclofenac na madawa mengine ya maumivu.
2.Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi

KAZI ZA FIGO
1. Kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu, kusaidia kuhifadhi,kudhibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini.
Figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.
2. Kusaidia kutengeneza kiasili cha erythropoletin ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, hupokea asilimia 25 ya damu na kila figo ina chembechembe hai ndogo milioni moja, pia kusaidia kudhibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).
AINA ZA UGONJWA WA FIGO.
Zipo Aina mbili za Ugonjwa wa figo

1.Aina ya `kwanza figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla na muda mfupi.
2. Aina ya pili ni ile ya figo kushindwa kufanya kazi polepole na kwa muda mrefu.Figo huharibiwa taratibu na kuendelea kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi kadiri siku zinavyokwenda.Figo kushindwa kufanya kazi polepole na kwa muda mrefu.
SABABU ZA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA GAFLA
1. Kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye figo, kemikali za mwilini au kushambuliwa na sumu. Sababu za figo kushindwa kufanya kazi ghafla
2.Ugonjwa wa moyo, moyo kushindwa kusukuma damu kwa ghafla, au waliougua maradhi ya moyo kwa muda mrefu.
3.Sababu zinazofanya figo ishindwe kufanya kazi taratibu na kwa muda mrefu na hatimaye kushindwa kabisa kuwa ni presha kuwa juu, kisukari, magonjwa yanayosababishwa na bakteria, HIV, saratani na sumu mbalimbali zinazoingia mwilini.

DALILI ZA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI.
1.Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kiasi cha mkojo, kushindwa kupumua, kusikia kichefuchefu, kutapika na kuvimba miguu.
2.Dalili nyingine ni maji kujaa mwilini, madini ya mwili kuwa juu hasa ya ‘potashiamu’, asidi nyingi, matatizo katika moyo, ubongo, kukosa hamu ya kula na kudhoofika mwili.
3. Dalili nyingine kwa wagonjwa ambao hawagunduliki mapema ni kuvimba macho wakati wa asubuhi na uvimbe kupungua baadaye.
4. Dalili nyingine ni kuvimba miguu asubuhi, kupungukiwa damu mwilini kama dalili za kwanza (kwani figo ikishindwa kufanya kazi ya kusaidia kutengeneza damu).
TAFADHALI SHARE NA WENGINE ILI ELIMU HII IWEZE KUWA SAIDIA

No comments:

Post a Comment