Search This Blog

Wednesday 24 May 2017

MAMBO AMBAYO HUWEZA KUMTOKEA MWANAMKE MWANZONI MWA KIPINDI CHA UJAUZITO

Image result for pregnant woman Wanawake wengi hukabiliwa na mabadiliko mbalimbali ya kimwili na kisaikolojia pale wanaposhika ujauzito.
Mabadiliko hayo hutokana na homoni za uzazi kuzalishwa kwa wingi zaidi. Miongoni mwa mabadiliko hayo katika kipindi hiki cha


ujauzito ni pamoja na mama kuhisi kuchoka zaidi ya ilivyokawaida.
Katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito, mwanamke anaweza kujikuta akihisi hali ya uchovu mara kwa mara. Na hii inaweza kuwa uchovu wa kawaida au kuchoka sana zaidi ya kawaida ukilinganisha na kipindi ambacho hakuwa na ujauzito.
Mama mjamzito pia huweza kutapika hasa nyakati za asubuhi, hii si hali ya ajabu kwa wanawake wengi wakati wa kipindi cha mwanzo wa ujauzito, lakini wengi pia hujikuta wakiondokana na hali hiyo kadri mimba inavyokuwa.
Hata hivyo mama mjamzito anashauriwa kumuona daktari endapo ataona anatapika sana karibu siku nzima.
Hali nyingine ambayo huweza kujitokeza kwa mama mjamzito katika kipindi cha mwanzo ni kukojoa mara kwa mara. Hii ni kutokana na tumbo la uzazi kuanza kukua na kukandamiza kibofu cha mkojo na hivyo kuleta hali ya kukojoa mara kwa mara.
Matiti kuvimba na kuuma, hii hali huchangiwa na mabadiliko ya
kihomoni kwa sababu wakati huo pole pole matiti huanza kukua na kujiandaa kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto hivyo mabadiliko hayo huchangia kuleta hali ya matiti kuvimba na kuuma.
Kukosa hedhi hii ni moja ya ishara kuu ya ujauzito na kwa kawaida haitegemewi mwanamke mjamzito kuendelea kupata siku zake za hedhi isipokuwa kutokwa na damu kidogo (matone kidogo kwenye
nguo za ndani kwa siku moja au mbili). Mwanamke anapopata hedhi ya kawaida au kutokwa damu nyingi wakati wa ujauzito huashiria hatari ya ujauzito kutoka, hivyo ni muhimu kwenda hospitali mapema pale hali hiyo inapojitokeza.
Kukosa hamu ya baadhi ya vyakula, kipindi hiki mama huweza kuacha kupenda baadhi ya vyakula au vinywaji hata kama hapo awali kabla ya ujauzito alikuwa anavitumia na wengine hujikuta wakichukizwa na baadhi ya harufu pia.
Pia kuna baadhi ya kinamama wanapokuwa katika hali hii ya ujauzito huweza kuwa wepesi wa kununa na kukasirika na hali hii husababisha hata wengine kujikuta wakiwachukia wenzi wao pia. Hivyo inashauriwa kuwachukulia katika hali hiyo endapo ikiwa hivyo.
Mabadiliko yote hayo hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, hata siku kwa siku na unapopata mabadiliko yanayokupa hofu ni vizuri ukaonana na daktari wako haraka

No comments:

Post a Comment