Search This Blog

Thursday, 20 October 2016

BILHARZIA (kichocho)

Ufahamu Ugonjwa Wa Kichocho



Kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo ambayo humpata mtu anapotumia maji yaliyo na vijidudu hivyo vya maradhi hususan katika nchi za kitropiki (yaani zenye hali ya joto jingi). Bilharzia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Aina za minyoo inayosababisha ugonjwa wa kichocho kikuu kinachomuathiri binadamu ni hii ifuatayo:
 Moja, Chistosoma mansoni ambayo imeenea katika nchi 53 na kwenye maeneo kadhaa ya Afrika, Caribbean, mashariki mwa Mediteranean na Amerika ya Kusini.
Aina ya Pili ni Chistosoma japonicum/ chistosoma mekongi, inayoathiri utumbo.
Tatu ni Chostosoma intercalatum- inayojulikana kama urinary bilharizia.
Na nne ni ile ya Chistosoma haematobium au urinary bilharzia, ambayo inaziathiri nchi nyingi za Afrika .
Ugonjwa wa kichocho unahesabiwa kuwa ugonjwa wa pili unaonea kwa wingi zaidi katika nchi zenye joto jingi.
Viini vya ugonjwa wa kichocho vilivyokomaa huishi katika mishipa kwenye kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa na kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa. Mayai yanapokutana na maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi ambao hupenya na kuingia ndani ya konokono wa majini.
Aidha viluwiluwi hawa hukuwa ndani ya konokono hao, kuongezeka na hatimaye kutoka. Ifahamike kuwa  viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya ndani ya ngozi ya mwanadamu na wakisha penya huingia hadi katika mishipa ya ini, ambako hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu cha mkojo na utumbo mpana.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka 3 na nusu, na vinaweza kuongezeka zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpana na kibofu husababisha madhara makubwa.
Hta hivyo iwapo ugonjwa wa kichocho hautatibiwa ipasavyo, unaweza kusababisha matatizo ya ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Aidha maambukizo yake yanaweza kuenea katika uti wa mgongo na hata wakati mwingine kuathiri ubongo.
Karibu watu milioni 600 duniani wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kichocho tafit zimeeleza.
Ugonjwa unasababishwa na Nini?
Matatizo yafuatayo yanapelekea watu kupatwa au kuambukizwa ugonjwa wa kichocho: Umaskini uliokithiri, ufahamu mdogo kuhusu ugonjwa huo, usafi duni wa mazingira tunamoishi au kutoka kwa watu wanaohama kutoka katika nchi nyingine ambazo ugonjwa huo umeenea n.k.
Katika siku za awali wakati vimelea vya kichocho vinapoingia katika mwili wa mwanadamu, kijipele hujitokeza na baada ya kupita mwezi mmoja au miwili, mtu aliyekwishaambukizwa huanza kujisikia hali ya kuchoka, homa, homa ya baridi, huwa na kikohozi kikavu, maumivu ya misuli, maumivu ya tumbo, kuhara, na hukojoa mkojo ulio na damu. Kipindi hiki huenda sambamba na ukuaji wa minyoo katika mwili wa mwanadamu na hujulikana kama homa ya Katayama.
Hata hivyo kuwepo kwa damu katika mkojo ni dalili tosha ya kuonyesha kwamba mtu huyo amepatwa na kichocho cha mkojo au kitaalamu hujulikana kama urinary bilharzias. Na iwapo mgojwa hatatibiwa, anaweza kupata madhara mengine makubwa katika ini na bandama.
Kichocho huathiri zaidi watu gani?
Watu wazima wanaojishughulisha na kilimo na wale walio katika sekta ya uvuvi wako hatarini zaidi kukubwa na ugonjwa wa kichocho.
Kichocho kinachoathiri kibofu cha mkono huwaathiri watoto milioni 66 katika zaidi ya nchi 54 duniani na katika maeneo mengi watoto walio na umri wa kati ya miaka 10 na 14 wanaambukizwa ugonjwa wa kichocho. Kimsingi maradhi haya huathiri ukuaji wa watoto na mahudhurio yao shuleni.
Mtu anatakiwa kumuona daktari iwapo atakuwa amesafiri katika eneo ambalo lina maambukizo ya kichocho, iwapo ngozi yake itagusana na maji yenye vimelea vya ugonjwa huo na iwapo atakojoa mkono ulio na damu.
Namna ya kuzuia ugonjwa wa kichocho
Ugonjwa wa kichocho unaweza kuzuiwa kwa urahisi iwapo kanuni za kiafya zitazingatiwa. Hata hivyo hadi sasa hakuna chanjo iliyopatikana ya kudhibiti ugonjwa huo.
Si maji yote ni salama kwenye maeneo yaliyo na ugonjwa huu. sehemu hatari zaidi za ugonjwa huo ni maeneo kama vile kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea.
Sehemu salama ni kama vile katika fukwe za bahari na zile zenye mawimbi ambazo si rahisi kukuta konokono wa majini. Mabwawa ya kuogelea ni salama iwapo yatanyunyiziwa dawa ya klorini.
Ili kuweza kukabiliana na kuzuia maambukizo ya ugonjwa wa kichocho, masuala yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa: Miongoni mwao ni kuacha kuoga kwenye maji yaliyotuama kama vile ya kingo za mabwawa, mito n.k.
Licha ya hayo pia hakikisha kuwa maji ya kunywa ni salama kwa kuyachemsha na kuyachuja ili kuuwa vijidudu vya maradhi. Unaweza pia kuchemsha maji ya kuoga angalau kwa nyuzi joto 65 kwa muda wa dakika tano.
Maji yaliyohifadhiwa kwenye tanki kwa muda usiopungua masaa 48 ni lazima yawe salama kwa ajili ya kuogea. Kama unalima, unashauriwa kuvaa mabuti marefu ya mpira, Mtu anapaswa kumuona daktari baada ya kuwa na dalili za ugonjwa na yeye ndiye atakayemuainishia dawa za kutumia.
Ni matarajio yangu kwamba tukifuata kanuni na misingi yote hiyo ya kiafya niliyoitaja, tutashinda vita dhidi ya maradhi ya kichocho.

Prepared by 
     DR Salim Amour
Cardio-thoracic suergeon

1 comment: