Search This Blog

Friday, 16 October 2020

𝐓𝐀𝐓𝐈𝐙𝐎 𝐋𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐖𝐀 𝐃𝐀𝐌𝐔 𝐏𝐔𝐀𝐍𝐈 (𝐂𝐡𝐚𝐧𝐳𝐨, 𝐌𝐚𝐝𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐧𝐚 𝐓𝐢𝐛𝐚)

Swala la damu kutoka puani ni la kawaida (Hutokea kwa watu wengi mara kwa mara hasa utotoni. Inaweza kukutisha lakini ni mara chache sana ikaonesha tatizo la kutisha /Kubwa

Pua huwa na mishipa mingi sana ya damu ambayo ipo nje nje sana hasa maeneo ya mwanzoni mwa pua na mwishoni ( Ndani ya pua)
Mishipa hii ni mirahisi sana kupasuka tena kwa haraka. Hali hii huwatokea zaidi watoto kati ya umri wa miaka 3 hadi 10

JE, SABABU NI ZIPI ZA DAMU KUTOKA PUANI ?

Kuna sababu nyingi , ila tatizo hili linapojirudia mara kwa mara basi linaweza kutueleza tatizo ambalo litahitaji uchunguzi wa daktari
  • Hewa Kavu (Dry air)......Hii ni sababu moja wapo , sehemu za ndani za pua zinapokosa unyevu na kua kavu kwa muda mrefu , basi itapelekea kuta za ndani za pua kupasuka na kupelekea damu kutoka
  • Matumizi ya madawa aina ya antihistamines na Decongestants kwa matatizo ya mzio (Allergies), mafua na matatizo mengine ya pua......Hii yaweza pelekea kuta za ndani za pua kuwa kavu na kupelekea damu kutoka

Sababu zingine za kawaida ni kama vile :
  • Kitu chochote kukwama ndani ya pua
  • Kemikali
  • Mzio (Allergy)
  • Pua kuumia kwa sababu zingine , kama vile ajali n.k
  • Chafya mara kwa mara
  • Hewa kavu au yenye ubaridi
  • Maambukizi katika mfumo wa upumuaji ( Hasa mfumo wa juu (upper respiratory infection) - Pua , koo la hewa n.k )
  •  Matumizi makubwa ya dawa aina ya Aspirin

SABABU ZINGINE AMBAZO NI MBAYA NI KAMA VILE :
  • Shinikizo la juu la damu
  • Matatizo ya kuvuja damu na damu kutoganda
  • Saratani

Mara nyingi sio tatizo la kushtua sana na halihitaji msaada wa kimatibabu . Isipokua tu kama damu itaendelea kutoka kwa zaidi ya dakika 20 au kama imetokea kwa sababu ya ajali basi unapaswa kutafuta usaidizi wa kimatibabu haraka
( may be a sign of a posterior nosebleed, which is more serious )

UNAWEZAJE KUTIBU TATIZO HILI ?

Matibabu yatategemea chanzo kilichopelekea damu kukutoka puani.
Tuanzie hapa :.....

DAMU KUKUTOKA SEHEMU YA MBELE YA PUA ( Kwa Ndani)

  • Kwanza kaa kitako , weka pamba au kitambaa safi kuziba matundu ya pua yako kwa dakika 10 hivi , inamia mbele kidogo na upumue kupitia mdomo
  • Usilale nyuma unapotokwa damu puani , hii itapelekea wewe kumeza damu na itapelekea kukwangua kuta za tumbo lako.
  • Baada ya dakika 10 , toa kitambaa au pamba ulizoweka puani na uone kama damu imekauka au bado inatoka . Kama bado inatoka endelea kuweka kitambaa au pamba puani

Kama hali itaendelea kwa dakika zingine , basi onana na daktari maana utakua umeshindwa kuzuia kwa njia za kawaida , yawezekana unatokwa damu sehemu za ndani zaidi.

  • DAMU KUTOKA SEHEMU ZA NDANI ZAIDI KATIKA PUA
Hapa utagundua kwamba damu inatoka na unaipata katika koo lako , yani unameza damu ila kwa puani huioni. Aina hii ni hatari zaidi
Hali hii huwezi itibu nyumbani , fanya kuwasiliana na daktari haraka au wahi hospitali

  • KAMA DAMU INATOKA KWASABABU KUNA KITU PUANI
Hapa daktari ndio atahusika kutoa hicho kitu kilichomo puani , kwahiyo nenda hospitali

  • CAUTERIZATION
Njia hii hutumiwa na madaktari kuzuia hali ya damu kutoka kwa wale wanaopata tatizo hili mara kwa mara. Huhusisha kuunguza mishipa ya damu katika pua ( Heating device au Silver nitrage yaweza tumuka)
Huhitaji kuelewa sana kuhusu hili , madaktari wanajua chakufanya

KUJIKINGA NA TATIZO HILI

Utajikinga baada ya kujua chanzo , ikiwa tatizo ni la kudumu na linajirudia mara kwa mara , basi onana na daktari ili akuchunguze na ajue kisababishi kati ya hivyo nilivyovitaja sehemu ya kwanza

Matumizi ya Saline spray au gel , yaweza saidia kuongeza unyevu puani na kupunguza ukavu unaopelekea damu kutoka

Zingatia matumizi yasiyomakubwa ya aspirin na antihistamines , Ongea na mfamasia atakushauri vizuri kuhusu matumizi sahihi ya madawa

No comments:

Post a Comment