๐Uke kwa kawaida Una asili ya Asidi, uke Una PH kati ya 3.5 hadi 4.5. Kwa maana hiyo Uke hujilinda wenyewe dhidi ya maambukizi ya bacteria, fungus na vijidudu vingine ๐จ
Hivyo basi, sehemu ya ndani ya uke haihitaji uioshe wala kuisugua wala kuifanyia usafi wowote ule ๐จ
Sehemu unayopaswa kuosha katika uke ni sehemu ya nje (mshavu, kinembe n.k) , na utaziosha sehemu hizo kwa kutumia maji safi na sabuni zisizo na dawa wala harufu au manukato ( Mfano waweza tumia sabuni kama Jamaa , Dove nk )
๐WANAWAKE wengi huugua magonjwa kama Fungus, UTI, PID na maambukizi mengine katika tumbo la uzazi, kwa kufanya makosa machache tu kuhusu namna ya kujisafisha na kulinda afya ya uke
๐คZingatia mambo haya ya msingi
1. Usitumie sabuni zenye kemikali, manukato au dawa kuoshea uke, tumia sabuni za kawaida (Mfano, dove n.k ) na uoshe sehemu ya nje tu
Ukiosha sehemu za ndani za uke utajisababishia magonjwa kama bacterial vaginosis na hata fungus maana utaharibu Uasidi katika uke, ambao hufanya kazi ya kulinda uke dhidi ya maradhi
2. Ukiweza tumia maji ya vuguvugu kuoshea sehemu ya nje ya uke. Maji ya vuguvugu yanatosha kabisa hata kama hutotumia sabuni za kawaida . Ila unapokosa maji ya vuguvugu basi waweza tumia maji safi hata kama sio ya vuguvugu
3. Wakati wote hakikisha unajikagua na unajua uke wako unatoa ute wa namna gani, kila ute utokao una kueleza kuhusu afya yako ya mfumo wa uzazi ๐. Huoni ni kazi rahisi sana kufatilia afya yako ya uke?
4. Ikiwa ute unaokutoka ni mweupe (Sio mara zote ) , njano, kijani au kahawia, basi huashiria kuwa unamagonjwa, mfano bacterial vaginosis, trichomoniasis (ugonjwa wa zinaa) , PID n.k , hapo ni vema uonane na daktari.
5. Uke huwa na harufu yake ya kipekee, nikawaida kabisa uke kuwa na harufu, lakini endapo harufu hiyo ya kawaida itabadilika basi ni dalili kubwa kabisa kwamba unaugonjwa. Mfano harufu kama shombo ya samaki hii huashiria kuwa Una ugonjwa unaitwa bacterial vaginosis (Hutokea pale ambapo bacteria wabaya huzidi na wale wazuri hupungua sana)
6. Hakikisha unajisafisha kutoka mbele kwenda nyuma. Fanya hivo kila ujisafishapo
Kwasababu sio miwasho yote au maumivu ukeni husababishwa na fungus, bali dalili hizo zaweza sababishwa na ugonjwa unaoitwa BV (Bacterial vaginosis ) au magonjwa ya zinaa (mfano Trichomoniasis) n.k
8. Sio mda wote unavaa chupi au boxer ukidhani unalinda usalama na afya ya uke, sehemu hizo zinahitaji hewa na zisibanwe mda wote paache papunge upepo ๐ . Ukiwa nyumbani na umekaa mazingira tulivu au usiku ukiwa umelala pendelea kuwa free, usivae nguo za ndani, labda tu kama utakua katika hedhi ๐จ
9. Hakikisha unatumia nguo za ndani ambazo zimetengenezwa kwa pamba. Hizi husaidia hewa kupenya na kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya fungus.
10. Badilisha nguo ya ndani kila unapotoka katika shuguli zako za kila siku, au unapotoka katika shuguli Fulani na ukahisi jasho limekutoka sana, basi ni vema kubadili nguo ya ndani baada ya kuoga.
11. Unapokua mkavu ukeni wakati wa tendo , usitumie tu mafuta yoyote yaliyopo mbele yako. Mfano wapo ambao hutumia mafuta ya mgando kama vile vaseline, babe care n.k. Mkumbuke hayo mafuta hayaendani kabisa na wala hayakutengenezwa kwa matumizi hayo, uke unahitaji uasidi na mazingira yake kutovurugwa ili usipate maambukizi ya fungus au bacteria. Badala yake nenda pharmacy na uulizie vilainishi vyakusaidia wakati wa tendo, utapatiwa
12. Ukiona Mabonge makubwa makubwa ya damu wakati upo period, onana na daktari akusaidie. Hali hiyo huweza sababishwa na uwepo wa uvimbe katika tumbo la uzazi, au tatizo la endometriosis . Zipo dawa za kukusaidia, kama hormonal replacement therapy
13. Pendelea kupima afya yako mara kwa mara. Jambo hilo litakusaidia uepukane na maambukizi sugu, na kutatua tatizo lako mepema. Mfano magonjwa kama UTI, BV, yasipotibiwa mapema basi huweza kuleta madhara makubwa .
Note : Sio kila Ute mweupe /Kijivu/kahawia unaokutoka ukeni ni kwasababu unaumwa hapana , ila endapo unakutoka mwingi kiasi cha kulowesha nguo zako za ndani ni tatizo , muwasho , maumivu nk
UMEJIFUNZA NINI? Au UMEPENDA NINI ?